RAIS MAGUFULI APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI WA MCHANGA

Rais Dkt.John Magufuli amepiga marufuku usafirishaji mchanga kutoka kwenye machimbo ya madini  kwenda nje ya nchi.
Rais MAGUFULI ametoa agizo hilo Mkoani Pwani wakati wa kuweka jiwe la Msingi  Ujenzi wa Kiwanda cha kutengenezea marumaru cha  Goodwill Ceramic kilichoko Mkuranga,  mkoani Pwani.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli yupo katika ziara ambayo imeanza leo, katika mikoa ya kusini. Ambapo pia alipata nafasi ya kuwasalimia wananchi wa Nangurukulu alipokuwa njiani kuelekea mkoani Lindi kuanza ziara yake.

Rais Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ujenzi wa kiwanda cha Vigae kilichopo wilayana Mkuranga.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment