AWAMU YA PILI YA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUPITIA UREMBO MKOANI DAR YAHITIMISHWA LEO

Taasisi ya Manjano Foundation leo imehitimisha mafunzo ya awamu ya pili ya ujasiriamali kupitia urembo ambayo yalianza kufanyika mwaka jana yakitolewa na taasisi ya Manjano Foundation huku mdhamini wake mkubwa akiwa ni Shear Illusions Africa. 

Mafunzo hayo yamekuwa yakiwasaidia wanawake kuepukana na ugumu wa ajira na maisha kwa ujumla, kwani yanawajengea uwezo wa kuanzisha biashara kwa kutumia mtaji mdogo huku ujuzi ukiwa ni hazina kuu ambayo wanaipata kupitia mafunzo hayo.

Mradi huu pia umelenga kuwanufaisha wanufaika hawa kupitia vipodozi pendwa vya Luvtouch, ambapo watapata fursa ya kuunganishwa na taasisi za kifedha na kupata mkopo nafuu usio na riba kwa lengo la kuanzisha biashara kupitia vipodozi hivyo vya Luvtouch.


Wahitimi wa mafunzo ya ujasiriamali kupitia urembo wakikwa tayari wamepata vyetu vyao kwa pamoja wakiwa na mwalimu wa urembo (Kushoto) Bi Lidya Mwangi Ndiba na Shekha Nasser mkurugenzi wa Shear Illusions Africa (kulia) 



Baada ya mafunzo hayo wanawake ambao wamepata fursa ya kushiriki walimshukuru mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Shear Illusion Bi Shekha Nasser kwa moyo wake wa kupenda kuwasaidia wanawake wenzake. 

Katika picha ya pamoja ni washiriki wa mafunzo hayo ya ream makers wakiwa na mkurugenzi mkuu wa Shear Illusions ambaye pia ndiye mwasisi ya taasisi hiyo ya Manjano Foundation.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment