UKAME WADHOOFISHA HALI YA USALAMA NCHINI KENYA



Ukame unaoendelea katika bonde la ufa nchini Kenya umesababisha kuongezeka kwa mahitaji ya malisho miongoni mwa wafugaji katika bonde la ufa. Jamii za wafugaji zinazopatikana katika bonde hilo ambazo ni  Pokot na Tugen zimekuwa zikiingia katika migogoro mara kadhaa kutokana na kugombania maji na malisho ya mifugo yao. 

Inasemekana kuwa maua ya wanasiasa wawilili  Fredrick Cheretei na Simon Pepee ambao wote wanatoka katika jamii ya wapokot katika kaunti ya Baringo katika bonde hilo la ufa kunaweza kuongeza kasi ya migogoro inayotokea kati ya jamii hizo mbili.

Kutokana na mauaji hayo msemaji wa Kaunti hiyo ya Baringo Bwana William Kamket amesema, "tunawapa siku mbili" endapo  wakosaji ambao hawajagundulika wala kukamatwa hawatatajwa, basi hawatakuwa salama. 

Kutokana na kutokea kwa matukio hayo wananchi wamemtaka rais anayekaimu kwa sasa bwana   William Ruto kupitisha sheria itakayompa polisi ruhusa ya kumfyetulia risasi mhalifu. 

Pia shirika la msalaba mwekundu limesitisha zoezi la utoaji misaada kutakana na kushambuliwa na baadhi ya watu wenye silaha katika maeneo ya bonde hilo. 
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment