Seli nyekundu hutengezwa katika
maabara lakini tatizo ni kiwango kinachohitajika. Kundi moja la wanasayansi
katika chuo kikuu cha Bristol pamoja na idara ya damu na upandikizaji
limetengeza mbinu ya kuzalisha kiwango kikubwa cha damu.
Damu hiyo ya maabara itakuwa bei ya juu ikilinganishwa na damu
ya kawaida, kwa hivyo itatumiwa miongoni mwa watu wasio na aina ya damu.
Mfumo wa zamani ulishirikisha kutumia kiini shina kinachotengeza
seli nyekundu za damu katika mwili na kuzibembeleza kuzalisha seli kama hizo katika
maabara. Hatahivyo kila seli huchoka haraka na kushindwa kuzalisha zaidi ya
seli nyekundu 50,000.
Mbinu iliotengezwa na kundi hilo la wanasayansi wa Bristol
inalenga kuzishika seli shina mapema wakati zinapokuwa kwa wingi ambapo hatua
hiyo hujulikana kama kuzifanya seli hizo kuishi milele, wakati watafiti
wanapozipata aina hizo za seli huzifanya kuwa seli nyekundu.
Daktari Jay Frayne mmoja ya watafiti wa kundi hilo alisema:
Tumeonyesha uwezo wetu wa kuzalisha seli nyekundu zinazoweza kutumiwa katika
hospitali.
0 comments:
Post a Comment