ALICHOKIANDIKA PROF. SHIVJI BAADA YA NAPE KUTEMBEA JUU YA MIGONGO YA WATU JIMBONI KWAKE



Mtaalamu wa sheria kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Prof. Issa Shivji ameandika maoni yake katika ukurasa wake wa Twitter kwa kila alichokifanya Mbunge wa jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye jana alipokuwa katika mkutano wake na Wananchi wa jimbo hilo.


“Angekataa, Nawashukuru sana mama zangu nilijitolea kuwahudumia kuwa chini yenu kama mtoto wenu siyo kuwakanyaga” ameandika Prof. Shivji
Nape Nnauye alitembea juu ya migongo ya wamama ambao walilala chini lengo alipokuwa kwenye mkutano na wananchi wake siku ya Jumamosi ya Tarehe nane mwezi wanne.  

Mbunge wa jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye akitembea juu ya migongo ya akina mama waliokuwa wamelala chini kwa lengo la kumpa heshima mbunge huyo

Hata hivyo inaelezwa kwamba kupita juu ya migongo ya watu na kuwakanyaga ni mila miongoni mwa mila za watu wa kusini ambazo huwa zinaonesha heshima kwa mtu huyo ambaye anawakanyaga watu migongoni. 
Mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nnauye amesema kitendo cha yeye kupita juu ya wamama waliolala chini ni mila ya kwao ambayo hufanyika kuonyesha heshima kubwa.

Mbali na tukio hilo kubwa ambalo liimfanya mbunge huyo kushindwa kuzuia hisia zake hadi kuangusha machoz, Nape amezungumza mambo mengi na wananchi wa jimbo hilo, amesitiza ufuatiliaji juu ya mambo kadha yanayoendelea nchini ikiwemo hili la utekaji na vitisho ambavyo watu wamekuwa wakitoleana.

Mbunge huyo pia leo alipata nafasi ya kuzungumza na wazee wa jimbo hilo waliomuita na kumuombea dua ya Baraka kabla hajarudi kuelekea bungeni.


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment