NAPE AELEZA SABABU ILIYOMFANYA ALIE KWENYE MKUTANO

Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye ameeleza sababu iliyomfanya aangue kilio mbele ya wananchi wake wa jimbo la Mtama jana alipokuwa katika mkutano wake na wananchi wa Mtama.



Mbunge huyo amesema kwamba alishindwa kujizuia pale alipoona akina mama wamejipanga wakiwa wamelala chini na kumtaka atembee juu yao, kitendo hiko kwa jamii za watu wa kusini kinaelezwa ni kitendo cha heshima kubwa ambayo huoneshwa mtu, na huchukuliwa kuwa ni dharau kubwa na wanajamii endapo mtu atatakiwa kufanya hivyo na akakataa.

“Kwa mila za kusini tendo hili ni la heshima kimila na ukikataa ni sawa na dharau kubwa kwa waliokufanyia, hivyo ndio maana nililizwa” ameandika Nape 

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment