Mvua zinazoendelea kunyesha
nchini zimeendelea kuleta maafa kwa wananchi, ambapo wilayani Chalinze mvua
ambayo imeambatana na upepo mkali imeharibu barabara katika eneo la Buyuni na
kukwamishwa shuhuli za mawasiliano na usafiri kwa wakazi wa kata ya Vigwaza na
Mwavi katika wilaya hiyo.
Mbunge wa Chalinze Mhe.
Ridhiwani akitazama barabara ya Vigwaza-Mwavi ambayo imeharibiwa na mvua
|
Kutokana na adha hiyo wakazi
wa Vigwaza na Mwavi wamelazimika
kuvushwa na watu ambao wanawabeba mgongoni kwa gharama za Tsh. 2,000
hadi 3,000 ambazo ni kubwa kwa wakazi wa
maeneo hayo, lakini pia magari yameshindwa kupita katika eneo hilo kutokana na
uharibifu huo mkubwa.
“Barabara ni mbovu kama
mnavyoiona, haipitiki, watu tunapata shida kufuata mahitaji ya nyumbani, tatizo
ni mkandarasi, barabara iimejengwa bila kuwekwa makaravati” alisema Zainab Zuber
mmoja wa wakazi wa maeneo hayo aliyekuwa
njiani kuelekea Mwavi.
Hata hivyo adha hiyo imeleta
neema kwa baadhi ya vijana wa maeneo hayo ambao waliitumia adha hiyo kama fursa
kwa kufanya kibarua cha kuwavusha watu tangu April 7 ambapo mvua zilianza
kunyesha, mmoja wa vijana hao Rashid Juma alisema wanavusha watu kwa maelewano
kulingana na uwezo wa mtu
“Tunapata fedha kulingana na
kichwa cha mtu au pikipiki, kila mtu mmoja 3,000 au 2,000 na pikipiki 5,000”
alisema Rashid
Baadhi ya wakazi wanaotumia
barabara ya Vigwaza-Buyuni wakipita katika barabara hiyo kwa shida kutokana na
uharibifu uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo hayo
|
Mbunge wa jimbo la Chalinze,
Mhe. Ridhiwani Kikwete alitembelea eneo hilo na kujionea athari ambazo zimezotokea
katika eneo hilo kutokana na mvua. Ridhiwani alisema hali iliyopo inawapa
wakati mgumu wakazi wa maeneo hayo na kuahidi kuifikisha kero hiyo bungeni na
katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze ili lifanyiwe kazi.
Mbunge wa Chalinze Mhe.
Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishI wa habari juu ya uharibifu
uliotokana na mvua ziazoendelea kunyesha jimboni kwake.
|
0 comments:
Post a Comment