Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harysson Mwakyembe ametembelewa na Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mousa Farhan ofisini kwake mjini Dodoma. Balozi wa ran hapa nchini ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuimarisha mahusiano kai ya nchi hizo mbili na kuahidi kukuza ushirikiano baina ya nch7=I hizo mbili katika maeneo ya sanaa na utamaduni.
Hayo
yamesemwa na Balozi Mousa ikiwa ni siku chache tangu maonesho ya wiki ya
Utamaduni ya Shiraz kufanyika kwa mua wa miezi mitatu iliyopita ambapo maonesho
hayo yalifanyika mjini Dar es Salaam na visiwani Zanzibar na kuwakutanisha
pamoja raia wa Tanzania na Iran.
Balozi
huyo pia amemuahidi waziri Mwakyembe kwamba wako tayari kusaidia na kubadilishana
uzoefu na Tanzania katika tasnia ya filamu na sanaa, pia Balzoi huyo ametoa
mwaliko kwa Tanzania kushiriki kwenye maonesho ya wiki ya Utamaduni ya Shirazi
yatakayofanyika nchini Iran siku za karibuni mwaka huu.
Naye
waziri Mwakyembe amemshukuru Balozi Mousa kwa kumtembelea na
amemhakikishiamushirikiano na urafikimkatika masuala ya Utamaduni na Sanaa, na
kwamba serikali itahakikisha inawasikiliza na kuwasaidia wasanii wa nchini
kutokana na fursa zitakazokuwa zikipatikana kutoka serikali ya Iran na
kujiendeleza katika filamu.
0 comments:
Post a Comment