Huko nchini
Uruguay kuanzia mwei Julai mwaka huu bangi itaanza kuuzwwa kwenye maduka ya
dawa na kuwa nchi ya kwanza duniani kuuza bangi kihalali. Mchakato wa
kuhalalisha matumizi ya bangi nchini humo ulianza mnamo mwaka 2013 baada ya
kupitishwa kwa sharia ya uuzaji na ununuzi wa bangi.
“Bangi
itauzwa kwenye maduka ya dawa kuanzia Julai” alisema Msaidizi wa Rais wa
Uruguay, Juan Andrr Roballo alipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari.
Bei ya
bangi itakuwa $1.30 kwa gramu moja,
na wauzaji wa bangi watatakiwa kujisajili nan i lazima wawe raia wa nchi hiyo
au wakazi wa kudumu, haitaruhusiwa kwa muuzaji kununua gramu 40 kwa kipindi cha
mwezi.
Mashamba ya
bangi yatasimamiwa na serikali japo kwa watumiaji wa bangi wataruhusiwa kupanda
majumbani mwao. Mpaka sasa tayari maduka 16 ya kuuza bangi yameshasajiliwa na
maduka mengI zaidi yanatarajiwa kusajiliwa.
Hata hivyo
wafanyabiashara wa bangi wameingia hofu juu ya kupata faida ya biashara hiyo
kwa kuwa tayari serikali imepanga bei ya kuuza bidhaa hiyo, pia wameonesha
kutokubaliana na serikali juu ya kupangiwa kiwango maalum cha kununua bangi kwa
mwezi, wametaka wasipangiwe juu ya hilo.
Katika iku za karibunii nchi kadhaa ikiwemo Canada, zimeripotiwa zikijaribu kuhalalisha matumizi ya bangi kwa sababu kadha ikiwemo kile kinachosemekana kuwa ni tiba ya kansa
0 comments:
Post a Comment