ALICHOKIANDIKA RIDHIWANI KIKWETE KUHUSU KUTEKWA KWA ROMA NA WENZAKE


Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete ameandika katika ukurasa wa Instagram kutokana na kutoweka kwa msanii Roma Mkatoliki na Moni ambao walitekwa siku ya Alhamis majira ya saa moja jioni katika studio za Tongwe ambako amekuwa akifanyia shughuli zake za muziki.

                       
Mbunge huto ameandika haya “Tabia hizi zinazoanza chipukia katika nchi vinapaswa kukemewa kabla havijamea na kuzaa matunda. Mungu amsaidie kijana Roma na Moni huko waliko” ameandika Ridhiwani

Ni siku tatu sasa tangu tukio hilo ambalo limewashtua wengi kutokea, wasanii wa muziki leo wamezungumza na waandishi wa habari pamoja na kujadili ni kwa namna gani wanaweza kufanikisha kupatikana kwa Mwanahiphop huyo.
Nayo serikali na vyombo vya usalama vimethibitisha kutoshikiliwa kwa msanii huyo na wenzake na vyombo vya usalama. Kamanda Sirro kesho anatarajia kulitolea ufafanuzi suala hili, ambapo awali ya yote jeshi la polisi limeomba kusaidiana na wananchi kutoa taarifa ili kusaidia kupatikana kwa msanii huyo. 
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment