Baadhi ya wabunge katika
bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania juu ya baadhi ya matukio ambayo
yanatokea katika nchi ya Tanzanai ambayo yamepelekea kuwepo kwa hali ya
sintofahamu kwa wananchi na wawakilishi wao juu ya mustakabali wa usalama wa
maisha yao.
Jana April 11 katika bunge
la Muungano wa Tanzania baadhi ya wabunge waliamua kutolifumbia macho na
kuliongelea suala hilo, wapo waliotoa ushahidi wa chombo cha usalama wa taifa
kuhusika moja kwa moja na baadhi ya matukio ya utekaji. Mbunge wa jimbo la
Nzega Mjini, Mhe, Hussein Bashe kupitia Chama Cha Mapinduzi alitoa ushahidi
kwamba yeye aliwahi kukamatwa na usala wa taifa na kuteswa,
“Mimi nimekamatwa na kuteswa
na Usalama wa Taifa. Nimenyanyaswa sana nchi hii. Ikibidi mnifukuze” alisema Hussein
Bashe
Hussein Bashe |
Hata hivyo ni siku chache
zimepita ambapo Bashe alisema kwamba wapo wabunge 11 ambao usalama wao upo
hatarini kutokana na kupokea jumbe za vitisho, na kusema kwamba yeye ni mmoja
kati ya wabunge hao ambao wamekuwa wakitumiwa jumbe za vitisho
Mbunge wa Sumbawanga mjnini
Mhe Hillary Aeshi naye alitoa ushahidi juu ya viitisho ambavyo amewahi kutolewa
na kupelekea kutoingia katika mkoa wa Dar es salaam,
“Mimi ni miongoni mwa
wabunge niliotishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar, na mpaka sasa mimi sikanyagi Dar
licha ya kuimisi sana” alisema Hillary Aeshi
Aeshi |
Lakini pia mbunge wa Jimbo la Chalinze alitoa ushauri kwa
serikali kutokaa kimya juu ya mambo kama haya ya sintofahamu ambayo yanawatokea
wananchi, na kwamba yapo baadhi ya mambo amabyo yakitolewa tamko huwatoa hofu
wasiwasi na wananchi,
“Hakuna sababu ya Mwigulu kuendelea kukaa kimya wakati
wananchi wanaishi kwa wasiwasi juu ya usalama wao. Kutoa kauli kunasaidia kutoa hofu” alisema Ridhiwani
0 comments:
Post a Comment