RAIS MAGUFULI AZINDUA UJENZI WA RELI YA KISASA

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli leo amezindu ujenzi wa reli ya kisasa itakayokuwa ikifanya safari zake kutoka jinni Dar es salaam hadi Morogoro, ujenzi wa reli hiyo unaanza mara moja baada ya kuzinduliwa kwake leo. Shughuli hiyo ya uzinduzi ilienda sambamba na uwekaji wa jiwe la msingi na ukataji wa utepe.

Rais Magufuli (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa reli ya kisasa, anayefuatia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akifuatiwa na Mke wa rais Mama Janeth Magufuli

Pindi mradi huo utakapokamilika utaweza kurahisisha shuhuli za usafiri kati ya Dar es salaam na Morogoro, ambapo reli hiyo itaka[okamilika itatumia nusu saa tu kusafirisha abiria na mizigo, lakini pia mradi huu utawanufaish7a zaidi ya watu laki sita pindi reli hiyo itakapokuwa ikijengwa na ajira milioni moja mara ujenzi wa reli hiyo utakapokamilika.

Treni zitakuwa na uwezo wa kubeba Tani 35  na ujenzi wa reli hii ya kisasa utachukua miezi 30 na utagharimu TZS trilion 2.8 ambapo pia rais wa Uturuki amekubali kutupa mkopo wa kujenga reli ya kisasa kutoka Morogoro hadi Dodoma na tayari ametuma wawakilishi kwa ajili ya mradi huo.

Mradi huo unategemea kuwanufaishwa wakazi waishio maeneo ambamo reli hiyo itakuwa ikipita, ambapo amesema kwa sasa ajira zote zitakazotoka wapewe wakazi wa Pugu, lakini pia mradi huu unatarajiwa kuwa na awamu ambapo awamu ya kwanza, ni Dar hadi Morogoro ambapo mpaka mradi utakapokamilika msafiri atatumia saa moja na nusu, awamu ya pili ni Dar hadi Dodoma masaa mawili na nusu, Dar hadi mwanza kwa masaa saba tu, na baadae reli hii itaenda hadi Burundi. 

Pia rais Magufuli amesema amemtaka mkandarasi kumaliza kazi ya ujenzi wa reli hiyo kabla ya miezi 30 ili watanzania waanze kutumia 
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment