Uhusiano kati ya Marekani na
Urusi umedhoofika zaidi tangu Donald Trump apate urais mwezi Jabuari mwaka 2017.
Hayo yamedhihirishwa na rais wa Urusi Vladmir Putin alipokiambia kituo kimoja
cha runinga kuwa imani kati ya nchi hizo mbili imepungua.
Waziri wa mashauri ya nchi
za kigeni wa nchi ya Urusi Sergei Lavrov alikutana na waziri wa mambo ya nje wa
Marekani Rex Tillerson siku kadhaa huko mjini Moscow, ambapo kumekuwa na
misukosuko kuhusu shambulio la kemikali nchini Syria.
Marekani ilifanya shambulio
la makombora takriban 50 nchini Syria kwa kile walichokidai kuwa kuipinga
majeshi ya Syria ambayo ilifanya shambulio la sumu, shambulio hilo lilipingwa
vikali na Urusi, na rusi ikatangaza kuisaidia Syria katika ulinzi wa anga lake.
Naye Marekani imeitaka Urusi
kuacha kuiunga mono seriakli ya Syria.
Mashambulizi ya Marekani
yamezua utata kuhusu sera za Marekani nchini Syria huku baadhi ya maafisa
wakitaka hatua kuchukuliwa dhidi ya Rais Assad.
0 comments:
Post a Comment