CCM YAWATAKA WANAOTUMBULIWA WASILALAMIKE


Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga amewataka makada waliyumbuliwa na Rais Dkt. Magufuli kuacha kulalamika na badala yake wakubali mabadiliko hayo na kuheshimu maamuzi ya yaliyochukuliwa na Rais dhidi yao.

Kanali Lubinga aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi mkoani Iringa
“Rais anapoteua kiongozi na kumpa dhamana ni kwamba anaona kuwa unahitajika, lakini inapofika mahali amekuondoa ujue mazingira yale huwezi kuyamudu na anakuokoa ili usipate laana. Baadhi ya viongozi wameondolewa madarakani, lakini wamebaki wakilalamika mitaani ovyo” alisema Kanali Lubinga.

Mbali na kuyasema hayo Kanali Lubinga hakutaja majina ya baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakifanya vitendo hivyo pindi wanapotolewa kwenye nyadhifa zao.

Hivi karibuni kumekuwa na kauli mbali mnali kutoka kwa viongozi kadha ambao wamtolewa kwenye nafasi zao walizoteuliwa na Rais Magufuli, lakini pia wananchi wamekuwa wakitoa hisia zao na maoni yao juu ya maamuzi hayo ya rais nay ale ambayo yamekuwa yakizungumzwa na baadhi ya viongozi ambao wametumbuliwa.


Haya yanatokea siku kadhaa baada ya aliyekuwa waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye nafasi yake imechukuliwa na Dkt. Mwakyembe, Nape ameonekana akiandika kwenye mitandao ya kijamii na hata kuitisha mikutano kuzungumza na wananchi kuhusu maamuzi hayo ambayo Rais ameyachukua. 
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment