Makamu wa Rais wa Marekani
Mike Pence amesema muda wa kuendelea kufanya subira na Korea Kaskazini
umekwisha, hii inatokana na kitendo cha Korea Kaskazini kutaka kurusha kombora
la majaribio ambalo hata hivyo lilishindwa kuruka. Makamu huyo wa Rais
ameyazungumza hayo alipowasili katika mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini,
Pence aliwasili mjini Seoul Jumapili muda mchache baada ya Korea Kaskazini
kufanya jaribio hilo la kurusha kombora.
Makamu wa Rais wa Marekani Mike
Pence (wa kati)
|
Bw. Pence aliwaambia
wanahabari alipokuwa katika kijiji cha Panmunjom siku ya Jumatatu huko Korea
Kusini, alisema "Kumekuwepo na kipindi cha subira, lakini kipindi hicho
cha subira kimemalizika."
Kumekuwa na majibizano
makali kati ya Marekani na Korea Kaskazini Siku za karibuni ambapo, amjibizano
hayo yameleta wasi wasi uimwenguni kwa kuhisi, pengine vita inaweza kutokea.
Korea Kaskazini imeishutumu
Marekani juu ya vitendo vyake ambavyo vinasemekana ni vya kiuchokozi na kuionya
Marekani juu ya hilo na kusema kwamba Korea Kaskazini ipo tayari kwa vita,
upande wa pili Bw. Pence amenukuliwa akisema kuwa jaribio la makombora la Korea
Kaskazini ni uchokozi.
Marekani imeahidi
kushirikiana na nchi ya Korea Kusini kuhakikisha panapatikana suluhu kwa njia
ya amani ili kuhakikisha usalama katika eneo la rasi ya Korea.
0 comments:
Post a Comment