Huko nchini China utawala wa
Beijing umeendelea na harakati zake zinazolenga kuzuia ueneaji wa itikadi kali
nchini humo kwa kuzuia ufugaji ndevu hadi zikawa ndefu kwa wanaume ambapo
utamaduni huu upo zaidi na unatekelezwa katika dini ya Kiisilamu ulimwenguni
kote. Kufuatia suala hili sheria zimepangwa kuanza kutumika katika jimbo la Xinjiang
magharibi mwa China.
Mbali na hilo, pia hatua
nyingine ambayo imepangwa kuchukuliwa ni kuzuia mavazi ya wanawake ambayo
yanaziba uso yanayojulikana kama niqab, haya yote yameelekezwa zaidi katika
jimbo la Uighurs ambako kuna idadi kubwa ya waislamu, ni mara kadhaa watu wa
jamii hiyo ya Uighurs wametaka kuwa na mamlaka huru na kusababisha kuwepo kwa
mvutano mara kadha baina ya watu wa jamii hiyo na maafisa wa polisi.
Wanaharakati ambao wanapinga
sharia hizo wanasema zinalenga kuangusha utamaduni wa jamii ya waisilamu
wanaoishi Uighurs
0 comments:
Post a Comment