Waandamanaji nchini Paraguay
wamevamia majengo ya bunge la nchi hiyo na kuchoma moto kwa kile kinachodaiwa,
bunge hilo kupiga kura za kurekebisha katiba na kuruhusu rais aliye madarakani Horacia
Cartes kuendelea kugombea tena.
Katika tukio hilo wapo
baadhi ya watu ambao walijeruhiwa baada ya polisi kujaribu kuwatawanya
waandamanaji hao katika eneo la tukio kwa kurusha maji ya kasi na kufyatua
risasi kwa lengo la kuimarisha usalama katika eneo hilo.
Waandamanaji hao wanadai ya
kwamba mabadiliko hayo yanaweza kuharibu misingi ya demokrasia katika nchi
hiyo, lakini yapo matumaini makubwa ya muswada huo kukubaliwa kutokana na Rais
huyo kuwa na idadi kubwa ya wabunge wanaotoka katika chama chake lakini pia
muswada huo uko mbioni kuelekea katika hatua ya pili ambapo utapelekwa katika
bunge la darasa la pili.
Sheria ya kutoruhusu marais
nchini Paraguay kutogombea mara mbili ilipitishwa mnamo mwaka 1992 ili kuondoa
kile kilichokuwa kikidaiwa ni udikteta wa rais kung’ang’ania kuendelea kubaki
madarakani.
0 comments:
Post a Comment