Peter Lijualikali ambaye ni
mbunge wa Kilombero kupitia tiketi ya CHADEMA amesema amepata heshima kwa
kifungo ambacho alikuwa nacho japokuwa alikuwa akipata mateso makali alipokuwa
gerezani, amesema kifungo hiko kimempa furaha kana kwamba amepata shahada ya
udaktari (PHD)
Alieleza chakula cha dagaa
ambacho alichokuwa anakula ya kwamba kilikuwa na mchanga nusu kikombe mara
baada ya kuoshwa “Tulikuwa tunakula ugali wa dona ambao kwa mtu wa kawaida
hawezi kula kwa sababu umechanganywa na magunzi” alisema Lijualikali
Alisema kuna sehemu ndani ya
gereza ambalo linaitwa siyaki shari, eneo hilo hutumika kuwaadhibu wafungwa
ambapo alipata kushuhudia mfungwa mwenzake ambaye alipigwa hadi kufikia hatua
ya kutambaa
Akiendelea kuzungumza
alisema kwa hadhi yake kama mbunge alipaswa kulazwa daraja la tatu ingawa
aliwekwa katika eneo tofauti na kuliacha daraja hilo walazwe watoto waa
viongozi, watuhumiwa wa meno ya tembo na raia wa China ambao hakutaja kesi
ambayo iliwapeleka gerezani.
“Magereza kuna madaraja
matatu la kwanza, la pili, na la tatu ambalo nilitakiwa kulazwa hummo ili
nipewe ulinzi kutokana na hadhi yangu” alisema Lijualikali
Lijualikali aliyasema hayo
jana mara baada ya kutoka nje ya jingo la Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam
alimokuwa akitumikia kifungo hicho na kuahidi kwamba vitendo vyote ambavyo hakuvitaja atakwenda kuvisema Bungeni Dodoma.
0 comments:
Post a Comment