HUU NDIO MSIMAMO WA LIGI YA EPL BAADA YA MANCHESTER KUILAMBA CHELSEA 2-0


Mchezo uliochezwa leo kati ya Chelsea na Manchester United katika uwanja wa Old Traford ambapo Manhester United ililinda heshima yake kwa kutofungwa katika uwanja wa nyumbani, kwa kupata ushindi wa Magoli mawili dhidi ya Mahasimu wao Chelsea.

Kocha wa Timu ya Manchester United Josee Mourinho ameusifu mchezo waliouonesha wachezaji wake na kusema kwamba walionesha mchezo mzuri.

Japo timu ya Chelsea imetoka kappa katika mchezo wa leo, lakini bado inashikilia nafasi ya kwanza ikiwa na jumla ya pointi 75, huku Manchester United ikishika nafasi ya tano ikiwa imepanda kwa pointi 60, ambapo ni tofauti ya ponti 15 kati ya timu hizo mbili.


Pia katika msimamo huo timu ya Liverpool imeonekana ikipanda huku Manhester City ikishuka daraja. Timu ya Sunderland imeendelea kushika mkia ikiwa na jumla ya pointi 21. 

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment