Rais Dkt. John Pombe
Magufuli ameomba waumini na wananchi wamuombee ili nchi iwe na umoja, amani, mshikamano na watu wenye kupenda kuchapa kazi, amezungumza hayo alipokuwa akishiriki ibada ya pasaka leo katika kanisa la Mtakatifu Petro akiwa
pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli.
Ibada hiyo imeongozwa na
Paroko wa Parokia ya Ostabei Padre Asis Mendokta na kuhudhuriwa pia na Askofu
mkuu wa jimbo kuu Katoliki la Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
na waumini wengine.
Kardinali Pengo amemuombea
Rais awe imara katika changamoto za kiuongozi anazokutana nazo, pia Kardinali
Pengo amesema Baraka zilizoletwa na Yesu Kristo aliyefufuka ni kwa ajili ya
watu wote na amemtakia Rais Magufuli heri ili matumaini ya Baraka hizo
ziwafikie watanzania.
Rais Dkt John Pombe Magufuli
akisali ibada ya Pasaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam
leo Aprili 16, 2017.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Mwili wa Bwana wakati wa ibada ya
Pasaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam.
|
0 comments:
Post a Comment