KOREA KASKAZINI YASHINDWA KUFANYA MAJARIBIO YA KOMBORA LAKE

Korea kaskazini imeshindwa kufanya jaribio la kombora lake baada a kombora hilo kuripuka siku moja baada ya maonesho ya silaha za kivita, kombora hilo lilijaribiwa kufyetuliwa lakini lilishindwa kuruka angani.



Ni siku moja imepita tangu nchi hiyo ya Korea Kaskazini kufanya maonesho ya silaha za kivita ambapo katika shuhuli hiyo, Korea Kaskazini ilitoa onyo kwa Marekani juu ya vitendo vyake vya uchokozi na kusema hawaogopi vitisho na ipo tayari kwa vita.

Matukio haya yanatokea ikiwa ni siku kadhaa tu tangu Marekani ipeleke meli zake za kivita katika Rais ya Korea.

Nalo jeshi la Marekani limesema kuwa kombora hilo lililoripuka, lilitakiwa kurushwa sekunde chache baada ya kufyetuliwa katika ufuo wa Mashariki mwa Korea Kaskazini.


Uhasama kati ya Marekani na Korea Kaskazini umezidi kuongezeka kila uchao kwa siku za hivi karibu ambapo kila mmoja kati yao amekuwa kionesha ubabe na jeuri ya kutaka kumuadabisha mwenziwe. 
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment