KATIBU WA WIZARA YA MAJI PROF. KITILA MKUMBO ATEMBELEA MTAMBO WA RUVU JUU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiaji Prof. Kitila Mkumbo ametembelea Mtambo wa Ruvu Juu uliopo eneo la Mlandizi Mkoani Pwani na kujionea kazi kubwa iliyofanywa na Serikali kupitia Wizara anayoiongoza.
Akiwa mtamboni hapo alipata fursa ya kushuhudia mtambo huo ukifanya kazi kama ilivyotarajiwa baada ya upanuzi wake kukamilika, ambapo hivi sasa mtambo una uwezo wa kuzalisha maji safi na salama kiasi cha lita milioni 196 kwa siku. 
Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara yake Mkoani hapo, Prof. Kitila amesema kwamba ziara hiyo ni muhimu kwake kwa kuwa amejifunza mambo mengi kuhusu namna maji yanavyopatikana ambapo ametoa pongezi kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika eneo hilo.
“Uwekezaji huu ni mkubwa sana uliofanyika katika eneo hili, uwekezaji huu unahitaji kutunzawa ili kudhibti upotevu wa maji”, alisema Prof. Mkumbo.

Amewataka Mameneja wa Miradi ya Maji kuhakikisha kuwa wanajiwekea malengo katika kuwahudumia wananchi na ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha kwamba wanayatunza maji wayapatayo kwakuwa upatikanaji wake ni mrefu na Serikali imewekeza fedha nyingi katika kuyapata maji hayo.


\

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment