Wasanii wa Bongo
Movie leo wameandama katika maeneo ya Kariakoo kushinikiza uuzwaji wa filamu
kutoka nje kwa madai ya kwamba, yanaua soko la filamu zao hapa nyumbani.
Ni siku chache tu zimepita
tangu wasanii hao wa bongo Movie kuwasilisha kilio chao kwa mkuu wa mkoa Paul
Makonda juu ya kuzuiwa kwa filamu hizo za nje ambazo zinasemekana ndizo
zinazoua soko la Filamu za hapa ndani. Mkuu wa mkoa Paul Makonda aliamuru
kutokuingizwa kwa CD za filamu ambazo haziendani na maadili ya mtanzania kutoka
nje.
Naye msanii Steve Nyerere
ameonesha kuwa tofauti na kile wanachoaminishwa wasanii wenzake wa bongo movie
kuwa maduka yanayouza filamu za nje yakifungwa filamu zao dndipo zitaweza
kununulika
“Tunaaminishwa kwamba
tukifunga maduka au tukizuia filamu za nje ndio za kwetu tutauza, uongo." Alisema
Seve Nyerere
Ameongeza kwa kusema, filamu
za nj zilikuwapo tangu siku za nyuma hivyo kuzuia filamu za nje si kukufanya
filamu za ndani kupata soko, suluhisho ni kuboresha kazi za filamu za ndani.
Pia amesema tatizo hili la kukosa soko kwa filamu za bongo kunatokana na
wasanii wenyewe kuwa kibiashara zaidi kunakopelekea muda mwingine kutozingatia
ubora wa filamu wanazotengeneza,
“ubora wa filamu zetu
watengenezaji wameshindwa kuwa wabunifu ili watu wanunue” alisema Steve Nyerere
0 comments:
Post a Comment