Abeid Amani Karume alizaliwa
katika kitongoji cha Pongwe kisiwani Unguja mnamo mwaka 1905 August 4, na kuwa mtoto
wa kwanza kati ya watoto watano wa Bwana Amani Karume na Bibi. Amina Bint Kadir.
Abeid Amani Karume alikuwa
na kiwango kidogo cha elimu, na aliwahi kufanya kazi kama baharia kabla
hajaingia kwenye siasa. Lakini pia aliondoka Zanzibar na kwenda nchini Ungereza
mjini London ambako alipata elimu ya masuala ya siasa na mambo ya kimataifa,
pia alipata nafasi ya kukutana na baadhi ya wanasiasa na viongozi kutoka nchi mbali
mbali za Afrika ikiwemo Kamuzu Banda wa Malawi ambapo karume alikomaa kisiasa
na kuwa na uwezo wa kukiimarisha chama cha Afro Shiraz Party lakini pia
kuboresha mahusiano na chama cha Tanganyika National Union party (TANU).
Zanzibar ilijipatia uhuru wake
wa kwanza kutoka kwa waingereza Desemba 10 1963 baada ya Zanzibar National
Party (ZNP) na Zanzibar People’s Party (ZPP) kushinda uchaguzi.
Karume alikuwa Rais wa
kwanza, na aliiongoza nchi ya Zanzibar baada ya mapinduzi yaliyofanyika
visiwani humo kumuondoa Sultan Jamshid aliyekuwa akiitawala Zanzibar hadi mwanzoni
mwa mwaka 1964 Januari, miezi mitatu badae Zanzibar iliungana na Tanganyika
kutengeneza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheikh Abeid Amani Karume kuwa
makamu wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Abeid Amani Karume alifariki
siku ya Ijumaa Tarehe 7 April 1972 kwa kupigwa risasi na alizikwa Tarehe 10
April siku ya Jumatatu
0 comments:
Post a Comment