Marekani imeishambulia Syria
kwa makombora takribani 50 katika kambi ya Homs nchini humo. Shambulio hilo
limekuja kutokana na shambulio la kemikali katika mji unaodhibitiwa na waasi
ambapo watu kadhaa wamepoteza maisha ikiwemo watoto, pia maafisa wa Marekani
wamepanga kuchukua hatua za kijeshi kutokana na shambulizi hilo la kutumia
kemikali.
Makombora hayo yamerushwa
kutoka katika meli za kivita za Marekani zilizo katika bahari ya Mediterania
Kufuatia shambulio hilo Rais
wa Urusi Vladmir Putin ametangaza kuipa ulinzi wa anga nchi ya Syria baada ya
Marekani kukiuka makubaliano ya kimataifa ya kuishambulia nchi hiyo. Hata
hivyomshirika wa Syria Urusi alitahadharisha kabla juu ya madhara yanayoweza
kutokea kutokana na hatua za kijeshi zitakazochukuliwa na Marekani.
Rais wa Marekani Donald
Trump jana alionesha kusikitishwa kwake kutokana na shambulio la sumu
lililofanyika jana na kuamuru kutekelezwa shambulio la makombora 50 dhidi ya
Syria na kuyataka mataifa yote kuomesha vitendo vya umwagaji damu nchini humo.
0 comments:
Post a Comment