Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
leo katika maadhimisho ya siku ya Afya Duniani ambayo huadhimishwa April 7 kila
mwaka duniani, ametoa takwimu ambazo zinaonesha kuwa Tanzania ina zaidi ya
wagonjwa 40,000 wanaougua ugonjwa wa Sonona.
Katika maadhimisho hayo kali
mbiu ya maadhimisho ya siku ya Afya Duniani mwaka huu ni “SONONA TUZUNGUMZE”
Waziri huyo amesema
kulingana na Takwimu za hivi karibuni za Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa sasa
Duniani kuna zaidi ya watu Milioni kwa
sasa Duniani kuna zaidi ya watu Milioni 300 wanaouguamugonjwa wa Sonona ambapo
idadi hiyo imeongezeka maradufu kwa 18% toka mwaka 2005 hadi 2015.
Kulingana na takwimu hizo
Tanzania ina wagonjwa wa Sonona 41,789 kwa mujibu wa H7\ali ya Afya ya magonjwa
ya aili ya mwaka 2015/2016. Pia WHO imeeleza kwamba Duniani, kati ya watu
watano mmoja anaugua ugonjwa huo.
SONONA
NI UGONJWA GANI
Sonona ni hali inayompata
mtu kimfumo usio na mpangilio kiufahamu inayoambatana na kujihisi huzuni, hali
hii inaweza kuchukua wiki mbili au zaidi.
DALILI
ZA UGONJWA SONONA
- Kukosa usingizi na hamu ya kula
- Kupenda kukaa peke na mara
nyingine kutaka kujidhuru hata kujiua
- Kuwa na kiwango kikubwa cha
msongo mkubwa wa mawazo na kukosa raha.
- Wasiwasi, shaka kupitiliza
kiasi na kuwa na hasira za haraka
- Kulala muda mrefu
- Uchovu na kukosa nguvu
Zipo sababu kadha wa kadha
ambazo zinaweza kumpelekea mtu kupata ugonjwa huu ikiwemo, kutokea kwa majanga
kama vile kuungua kwa nyumba, kubakwa, mafuriko, ugomvi katika familia na
mahusiano, kufiwa, kukosa huduma za kijamii na msaada n.k
Pia wataalamu wameeleza
kuwepo kwa sababu za kibaiologia, na kisaikolojia ambazo wakati mwingine
huweza kusababisha mtu kuupata ugonjwa huu.
0 comments:
Post a Comment