MALORI ZAIDI YA 400 KUTOKA TANZANIA YAZUILIWA NCHINI ZAMBIA


Zambia inayashikilia kizuizini malori 600 kutoka Tanzania yalipokuwa yakirudi kutoka Congo yalikokwendakubeba mbao, mpaka sasa maafisa kutoka nchini Tanzania wanatafuta njia za kidiplomasia za kumaliza suala hilo.
Nacho chama cha wamiliki wa malori Tanzania (Tanzania Truck Owners Assosiation TATOA) kimesema kuwa wanachama wake wamepoteza zaidi ya dola Milioni 6 katika miezi miwili ambayo madereva hao wamekamatwa na kuongeza kwamba maderea hao walifuata taratibu zote za ununuzi na mauzo ya nje na kuingia nchini Congo.
Mwenyekiti wa TATOA Angelina Ngalula amesema madereva zaidi ya 400 na wasaidizi wao wamezuliwa nchini humo.. Bi Ngalula amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam kwamba maafisa wa nchini Zambia wanaamini kwamba mbao hizo zinatoka Africa ya Kusini na si Congo kama inavyodaiwa. 
Pia Bi. Ngalula amedai kwamba madereva wanazo nyaraka zote zinazoonesha kwamba walifuata taratibuzote za ununuzi na usafirishaji wa mbao hizo kutoka Congo. 
"Madereva wametizmiza taratibu zote na waliruhusiwa kukatiza mpaka wa Congo na Zambia, lakini baadae walizuiliwa Zambia" Alisema Bi, Ngalula

Maafisa wa Tanzania wametoa wito kwa maafisa walioko katika ofisi za balozi za Tanzania nchini Zambia kuwasilisha suala hilo kwa maaisa husika nchini humo kwa lengo la kupata suluhu ya haraka.


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment