MAMA SALMA KIKWETE ALA KIAPO CHA UBUNGE

Wabunge wa Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimsindikiza Mama Salma Kikwende kwenda kula Kiapo

Leo April 4 2017 mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Rashid Kikwete ameapishwa bungeni kuwa mbunge wa viti maalum wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi. Kiapo hiko kimefanyika katika mkutano wa saba wa bunge la bajeti ambapo Spika wa bunge Job Ndugai amemuapisha rasmi.

Mhe. Salma Kikwete aliambatana na mummewe Dkt. Jakaya Kikwete bungeni ambapo uwepo wake ulisababisha shangwe zilizotoka kwa wabunge kwa kumshangilia Dkt. Jakaya kwa takribani dakika kumi nzima kwa sauti zilizosikika zikisema “Tumekumiss”

Mara baada ya kuapishwa Mhe. Slama Kikwete alipata wasaa wa kuuliza swali la kwanza, ambapo swali lake alilielekeza katika Menejiment ya Utumishi wa Uma na Utawala Bora.
Mama Salma ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, lakini pia anatajwa kuwa ni miongoni mwa wanawake wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini Tanzania.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment