Ripoti inayohusiana na
madawa ya kulevya na uhalifu ya mwaka 2016 iliyotolewa na Umoja wa Mataifa
inaonesha kuwa wanawake walioathirika na dawa za kulevya na kuambukizwa virusi
vya UKIMWI wamekuwa wakinyanyapaliwa na kutokuwa na usalama zaidi ukilinganisha
na waathirika wa kiume.
Hapa Tanzania wanawake wengi
wanaojihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya
ni wale walioshawishiwa kuingia katika lindi hilo na rafiki zao wa
kiume, hadi kufikia hatua ya kushawishiwa kufanya biashara ya ukahaba na
marafiki hao wa kiume.
0 comments:
Post a Comment