Marekani imesema iko tayari
kwa mazungumzo yenye lengo la kuondoa zana za nyuklia na Korea Kaskazini, lakini pia serikali ya Marekani imesema itatumia
nguvu za kijeshi ikiwa itahitajika kufanya hivyo.
Waziri wa mashauri ya nchi
za kigeni wa Marekani Rex Tillerson aliliambia baraza la usalama la umoja wa
mataifa kuwa Korea Kaskazini inalenga kufanya vitisho vya kushambulia nchi za
jirani yake kwa nyuklia. Hata hivyo waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa
China ambayo ni mshirika mkubwa wa Korea Kaskazini amesema makubaliano ya amani
ndio njia pekee.
Marekani tayari imepeleka
vikosi vya jeshi katika nchi za jirani na Korea Kaskazini ikiwemo Japan na
Korea Kusini huku hofu ikitanda zaidi kwa kile kinachodaiwa Korea Kaskazini
kutaka kushambulia nchi hizo za jirani, na kupelekea waziri wa mambo ya nje wa
Marekan Bw. Rex kuzitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo
nchi ya Korea Kaskazini.
“Ni wakati wetu kuchukua
hatua na kudhibiti hali hii, tishio la Korea Kaskazinila kufanya shambulio la
nyuklia dhidi ya Korea Kusini au Japanlinaweza kutokea” alisema TIllerson
0 comments:
Post a Comment