MGOMO WA MABASI YA ABIRIA WASITISHWA


Mgomo wa mabasi ambao ulikuwa ufanyike kuanzia kesho April 4 umesitishwa na mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, SUMATRA baada ya madai ya chama cha wamiliki wa mabasi ya abiria TABOA kusikilizwa na kufikia muafaka wa kurekebisha baadhi ya vipengele vya sheria vinavyofunganisha makosa kati ya dereva na mmiliki wa chombo cha usafiri.

Mkurugenzi mkuu wa SUMATRA, Gilliard Ngewe amesema kusitishwa huko kwa mgomo kumetokana na kikao cha waziri wa Mawasiliano, Uchukuzi na Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa kuhusu kutenganishwa kwa makosa ya dereva na mmiliki wa chombo cha usafiri.

Bw, Ngewe amesema, kanuini hizo zitaandikwa ndani ya siku 74 katika rasimu hiyo na, wadau wa usafirishaji wametakiwa kuendelea na shughuli za usafirishaji, na kwamba baada ya kufanya marekebisho ya rasimu ya kanuni itarudishwa kwa wadaukuweza kujadiliwa kwa ajili ya kuwasilisha bungeni.

Makamu Mwenyekiti wa wamiliki wa Mabasi TABOA, Abdallah Mohamed amesema wamekubaliana na SUMATRA kurekebishwa kwa baadhi ya kanuni za makosa kati ya wamiliki na madereva wa mabasi. 
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment