Huko mjini Mocoa nchini
Colombia watu 300 wamepoteza maisha
katika wilaya 17 zilizoko mjini Mocoa huko nchini Colombia kutokana na
maporomoko huku nyumba kadhaa zikiwa zimeharibika.
Inaelezwa kwamba maji ambayo
yalikuwa yameambatana na matope na mawe yameondoa kila kitukilichokuwa katika
maeneo hayo huku makazi ya watu yakiwa yamethirika zaidi.
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ametembelea eneo la tukio na amesema watapanga mpango wa kusaidia wakazi wa maeneo yaliyoathirika, amoengeza kwa kusema atafanya chochote kitakachowezekana kuhakikisha wote waliopoteza maisha kwenye maafa hayo watazikwa kwa heshima na taratibu zinazotakiwa huku akitangaza hali ya tahadhari katika maeneo hayo.
Wilaya ya San Miqeuel
imeathirika zaidi hadi kufikia kutoweza kutambulika. Eya wa Mocoa, Jose Antonio
Castro amesema wakazi wa maeneo hayo walionywa juu ya kuchukua tahadhari ya
kuhama maeneo hao japo wengi wao hawakufanya hivyo.
Jeshi la Colombia
likishirikiana na kikosi cha msalaba mwekundu wanafanya jitihada za uokoaji na
utoaji misaada ya haraka ikiwemo huduma ya kwanza kwa walionusurika na
maporomoko hayo.
Pia Chanselor wa Ujerumani
Angela Merkel ameeleza masikitiko yake na kutoa pole, Jumapili msemaji wa
serikali ya Ujerumani Georg Streiter akiwa mjini Berlin alisema Chansela
Merekel amesikitishwa na maafa hayo.
.




0 comments:
Post a Comment