MWIGULU AONGOZA KUAGA MIILI YA ASKARI NANE WALIOUAWA KIBITI

Waziri wa mambo ya ndani Mhe. Mwigulu Nchemba na naibu waziri wake Eng. Masauni leo jijin Dar es salaam wameshiriki katika shuhuli ya kuaga miili nane ya askai polisi ambao waliuawa siku ya Alhamis Kibiti mkoani Pwani, ambapo paoja na hilo waziri Mwigulu amewatangazia kiama wote waliohusika kwenye mauaji ya askari hao.  

Waziri wa mambo ya ndani, Mhe. Mwigulu Nchemba akitoa heshima za mwisho alipokuwa akiaga miili nane ya askari polisi leo jijini Dar es salaam, kulia kwake ni naibu wake Hamad Masauni

Waziri Mwigulu amezungumza hayo alipokuwa akiaga miili hiyo jijini Dar es salaam, ameongezea kwa kusema kuwa watu hao watakamatwa wote na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia
“Kitendo hiki cha mauaji kilichofanyika dhidi ya askari wetu hakivumiliki hata kidogo waliohusika tutawatafuta na kuwakamata” alisema Waziri Mwigulu

Pia aliwaomba wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa polisi ili kuweza kuwabaini waliohusika na tukio hilo. Ameitaka wizara kutoa fidia kwa ndugu wa askari hao na majeruhi bila kuwacheleweshea
“Naomba fidia kwa askari hawa tuliowapoteza wakitumikia taifa itolewe kwa haraka bila kucheleweshwa” alisema Waziri Mwigulu

Waziri wa mambo ya ndani, Mhe. Mwigulu Nchemba akiwafariji wafiwa kwa kuwapa pole katika shuhuli ya kuaga miili nane ya askari polisi leo jijini Dar es salaam

Mkuu wa jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu ametoa onyo kwa wale wote ambao wamekuwa wakishabikia matukio kama haya katika mitandao ya kijamii, nna endapo watabainika watakamatwa mara moja, pia alisema kuwa wananchi wa eneo hilo wanafahamu waliohusika kwenye tukio hilo na kuwataka washirikiane na polisi ili watuhumiwa wote wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya dola. 


Askari polisi waliopoteza maisha katika tukio hilo ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment