Baadhi ya wagombea wa kiti
cha urais nchini Ufaransa,(kutoka kushoto) Francois Fillon, Benoit Hamon,
Marine Le Pen, Emmanuele Macron na
Jean-Luc Melenchon
|
Leo April 23 nchini Ufarasa,
raia wa nchi hiyo wanatarajiwa kumchagua rais wa nchi hiyo ambapo uchaguzi huo
jumla ya wagombea 11 wakiwania nafasi hiyo huku wagombea wakuu wane wakionekana
kuwa na maarufu sawa.
Usalama umeimarishwa katika vituo vyote vya kupigia kura kufuatia tukio la shambulizi la kigaidi lililotokea katikati ya mi mkuu wa Ufaransa Paris hivi karibuni ambapo afisa mmoja wa afisa wa polisi aliuawa. Lakini japokuwa kumekuwa na ulinzi wa kutosha hofu ya ugaidi imezidi kutanda hususani katika mjii mkuu wa nchi hiyo Paris.
Imeelezwa kwamba polisi 50,000 na wanajeshi 7,000 wametumwa maeneo yote ya nchini Ufaransa kwa lengo la kuhakikisha usalama wa raia.
0 comments:
Post a Comment