RAIS MAGUFULI AWASILI DODOMA KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA MUUNGANO

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amewasili mjini Dodoma ambako atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 53 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ulizaa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maadhimisho ya muungano mwaka huu yatafanyika Dodoma ambako serikali inahamia, huku baadhi ya wizara zikiwa tayari zimekwishatekeleza agizo hilo la Mheshimiwa rais la kuhamia Dodoma
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na waziri mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Dodoma.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbali mbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Dodoma.

Rais Magufuli akisalima nan a Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili mjini Dodoma 

Maadhimisho hayo yatapambwa na maonesho ya ukakamavu na mbinu za medani katika kupambana na audi na kulinda amani ya nchi kutoka kwa kikosi maalum cha Makomandoo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), pamoja na maonesho hayo pia kutawepo na burudani kutoka vikundi mbali mbali vitakavyosherehesha. Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 53 ya muungano mwaka huu itakuwa  “Tupige vita dawa za kulevya na tufanye kazi kwa bidii”, huku ikiwa ni mara ya kwanza maadhimisho hayo kufanyika mkoani Dodoma. 

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment