WAZIRI MUHONGO AWATEUA WAJUMBE WANNE WA BODI YA UDHIBITI WA MKONDO WA JUU WA PETROLI

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo  amewateua wajumbe wanne wa bodi ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petrol (Petroleum Upstream Reguatory Authority- PURA) ambao wataongozwa na mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt. Adelardus Kilangi ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Wajumbe wa bodi walioteuliwa na Waziri wa Nishati na Madini nu; Dkt. Josephat Loto, Bwa. Yona Killagane, Bi. Beng’l Mazana Issa na Eng. Ramadhani M. Suleiman. Waziri Prof. Muhongo ameteua bodi hiyo kwa malmlaka aliyopewa chini ya kifungu Nambari 17(5) cha Sheria ya Petroli ya Mwaka\2015.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment