RAIS MAGUFULI AMTEUA PROF. RAPHAEL CHIBUNDA KUWA MAKAMU MKUU SUA

Prof. Raphael Chibunda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo April 24 amemteua Prof. Raphael Tihelwa Chibunda kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), ambapo kabla ya uteuzi huo Prof. Chibunda alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sayansi na Teknolojia katika wizara ya Elimu, Sayansi na Technolojia.
Imeelezwa kwamba uteuzi huo unaanza leo tarehe 24 April 2017, Prof. Chibunda anachukua nafasi ya Prof. Gerald Monela ambaye amemaliza muda wake

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment