Msajili wa vyama vya siasa
nchini, Jaji Francis Mutungi, amelaani na kukemea vikali vurugu zilizotokea
miongoni mwa wananchama na viongozi wa chama cha wananchi CUF zilizowahusisha
pia baadhi ya waandishi wa habari walioitikia wito uliotolewa kwao.
Taarifa iliyosainiwa na
msajili huyo na kusambazwa kwa vyombo vya habari inasema kuwa msajili huyo
anavitaka vyombo vya ulinzi na usalama katika nchi kulifanyia kazi tukio hilo
ili wahusika wafahamike na kuchukuliwa hatua mara moja, ‘’ninaomba vyombo vya ulinzi
na usalama katika nchi yetu kulifanyia kazi tuio hilo ili wahusika wafahamike
na kuchukuliwa hatua za kisheria’’. Imesema taarifa hiyo,
Aidha msajili Mutungi
amesema kuwa vurugu hizo zilionekana kuvunja Amani na utulivu na watu kuumizwa
jambo ambalo ni tofauti na tunu za taifa za Amani na utulivu huku akiwaasa
wanachama wa chama hicho kuwa pamoja na tofauti walizonazo kutulia kusubiri
uamuzi wa mahakama kwa kuwa tayari suala hilo liko mahakamani.
‘’ni ukweli usiopingika kuwa
suala la mgogoro wa uongozi katika chama cha CUF lipo mahakamani, lakini nikiwa
msimamizi wa sheria ya vyama vya siasa na kutambuliwa na kutambuliwa na jamii
na jamii kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa, nimelazimika kuwasihi wadau wa siasa
hususani wanachama wa chama cha CUF, kutambua kwamba kuwapo kwa shauri
mahakamani siyo fursa ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa Amani, kwani kwani
jambo hili ni uvunjifu wa sheria na linaleta sura mbaya kwa jamii’’. Iliongeza sehemu ya taarifa hiyo.
Hayo yamejili ikiwa juzi
tarehe 22 mwezi huu wa nne, akiwa katika mkutano na waandishi wa habari
uliotishwa na mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF wilaya ya Kinondoni bwana
Juma Mkumbi ambaye pia ni mjumbe wa baraza kuu la uongozi la taifa la chama
hicho anayedaiwa kumuunga mkono katibu mkuu wa maalim seif sharrif Hamad
kuvamiwa na watu wasiojulikana wanaozaniwa kuwa ni wafuasi wa mwenyekiti wa
chama hicho profesa Ibrahim Lipumba na kuvuruga mkutano huo uliofanyika katika
hoteli ya VINA iliyopo Mabibo Farasi jijini Dar es salaam
Katika tukio hilo watu
kadhaa walijeruhiwa ikiwemo waandishi wa habari na mmoja wa waliovamia kiasi
cha kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali mpaka alipookolewa na polisi na
kupelekwa katika kituo cha polisi magomeni
0 comments:
Post a Comment