Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo April 15 amezindua mabweni ya wanafunzi
katika chuo kikuu cha Dar es salaam, ambapo mabweni hayo yatahudumia jumla ya
wanafunzi 3,840 ambapo ni sawa na uwiano wa wanafunzi 192 kila jengo
Rais
Magufuli amesema Tanzania inaweza, hii imeoneshwa baada ya mabweni hayo
kukamilika ndani ya miezi nane. “Tukiamua tunaweza tukafanya watu wakaona miujiza”
alisema Magufuli
Pia
ameongeza kwa kusea watu walibeza kuwa Shilingi Bilioni 10 hazitoshi kujenga
mabweni hayo na yasingeweza kujengwa na watanzania. Amesema mafanikio hayo yawe
fundisho kwa viongozi wa serikali kutotoa fedha kwa wakandarasi wa nje na
kuwaacha wa ndani ambao gharama zake ni nafuu.
Makamu
mkuu wa chuo cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandara amesema mabweni hayo
yana jumla ya majengo 20 yenye ghorofa nne kila moja na jumla ya vyumba 12
katika kila ghorofa.
Pia
Profesa Rwekaza amesema kuwa chuo chake kimechangia ujenzi wa mabweni hayo kwa
utengeneza vitanda 1,920, droo 1,920, meza 1,920, magodoro 3,840 na vitanda 3,840
“Tutahakikisha
kuwa huduma zote muhimu kama vile cafeteria ya chakula, maduka kwaajili ya
mahitaji mbalimbali, zahanati, salon, kituo cha polisi na nyinginezo
vinapatikana hapa hapa,” alisema Profesa Rwekeza
Aliongeza
kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
kujenga taifa, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na. Mawaziri wote wa
wizara hizo, Profesa Makame Mbarawa, Dr. Hussen Mwinyi na Profesa Joyce
Ndalichako walikuwepo.
0 comments:
Post a Comment