IS YAKANUSHA KWAMBA WAPIGANAJI 90 WAMEFARIKI KUTOKANA NA SHAMBULIO LA MAREKANI



Wapiganaji zaidi ya 90 wa kundi la Islamic State waliuwawa na bomu ambao lilidondoshwa na majeshi ya Marekani siku ya Alhamis April 13 katika mapango ambamo wapiganaji hao hujificha. Taarifa hizo zimetolewa na maafisa wa usalama wa nchini Afghanstan ambapo idadi hiyo ni mara mbili ya ile iliyokadiriwa awali.

Kikundi cha wapiganaji cha Islamic State kimekanusha taarifa hizo na kusema kuwa hawakumpoteza mtu yeyote kutokana na bomu hilo lililolenga katika mapango na mahandaki ya chini Mashariki mwa Afghanistan.

Naye Kamanda wa jeshi la Marekani nchini Afghanistan, Jemedari John Nicholson, aliema kwamba Marekani ilitumia bomu hilo kubwa kutokana na mbinu madhubuti ya kijeshi. 

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment