VITA YANUKIA KATI YA MAREKANI NA KOREA KASKAZINI

Marekani yaonywa na Korea kaskazini kuacha vitendo vya uchokozi katika eneo la Korea, Korea Kaskazini imesema iko tayari kulipiza kisasi kupitia mashambulizi ya nyuklia. Kauli hiyo imetolewa wakati ambapo kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un alipohudhuria gwaride la heshima katika mji mkuu wa Pyong yang wakati Rais huyo akiadhimisha siku ya kuzaliwa babu yake, marehemu Kim II-Sung ambaye ndiye mwanzilishi wa taifa hilo.


“tumejiandaa kwa vita kamili”, alisema Choe Ryong-hae anayeaminika kuwa na uwezo mkubwa katika taifa hilo “Tuko tayari kulipiza kisasi na mashambulio ya Nyuklia kwa mbinu zetu dhidi ya shambulio lolote la Kinyuklia”

Katika gwaride hilo Bwana Kim alipata fursa ya kuonesha vifaa  vya kijeshi vya taifa hilo ambavyo kwa mara ya kwanza vilioneshwa. Vifaa hivyo ni vile vilivyotajwa kuwa manuwari za Pukkuksong, makombora ya masafa marefu yanayoweza kwenda urefu wa kilomita 1000. Pia wataalamu wanasema yapo makombora mawili ambayo yanaweza kurushwa toka bara moja hadi linguine japo bado haijulikani kama yamefanyiwa majaribio.


Maonesho na majaribio ya silaha za nyuklia nchini Korea Kaskazini kumeleta wasi wasi katika eneo la kusini ambayo pia uhasama unaoendelea kati ya Marekani na nchi hiyo. Siku za karibuni Marekani ilituma meli za kadhaa za kivita katika rasi ya Korea.  
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment