Rais wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru madakrati walioomba nafasi mia
tano za kwenda kuhudumu kazi ya udaktari nchini Kenya waajiriwe.
Agizo hilo limetoka mara
baada ya Mahakama ya Kenya kukubali ombi lililopelekwa mahakamani na chama cha
Madaktari nchini humo la kuzuia kuajiriwa madaktari kutoka nje badala yake
kutimiza madai yao. Kukubaliwa kwa ombi hilo kulipelekea Rais wa Kenya Uhuru
Kenyata kukubali kusaini maombi na mahitaji ya madaktari wa nchi hiyo ya
kuongezewa mishahara na kuboreshewa mazingira ya kazi.
"Serikali ya Tanzania
itakuwa tayari kushughulikia upya ombi la Serikali ya Kenya kupatiwa Madaktari
500, pale ambapo hakutakuwa na vikwazo vya kupeleka Madaktari wetu nchini
Kenya," amesema Bi Mwalimu.
Pia waziri Ummy Mwalimu amesema madaktari hao watapangiwa vituo vya kazi na taarifa itatangazwa katika tovuti ya wizara, ikijumuisha wataalamu wengine 11 waliopokea maombi yao na kukidhi mahitaji.
0 comments:
Post a Comment