Bi. Awa Dabo |
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imeliagiza Shirika la Umoja wa Mataifa la program ya Maendeleo
(United Nation Development Programs-UNDP) kwa upande wa Tanzania kumuondoa nchini
Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Awa Dabo
Serikali imefikia uamuzi
huo kutokana na Bi. Dabo kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya watumishi
wenzake na menejimenti ya shirika hilo na kupelekea kuzorota kwa utendaji wa
shirika hilo hapa nchini.
Baada ya kuthibitishwa
kuondoka kwa mkurugenzi huyo, serikali kupitia wizara ya mambo ya nje imetoa
rai kwa UNDP kuwakumbusha watumishi kuwa kipaumbele chao ni kufanya kazi na
serikali ili kufikia malengo ya mpango wa maendeleo endelevu.
0 comments:
Post a Comment