Meli ya kivita ya Marekani aina ya nyambizi yenye kuendeshwa kwa nguvu
za nyuklia imewasili katika bandari ya Busan, Korea Kusini wasiwasi ukiongezeka
kuhusu uwezekano wa Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora au
silaha za nyuklia.
Nyambizi hiyo, aina ya USS Michigan ni moja kati ya nyambizi mbili
zinazobeba makombora yanayoendeshwa kwa nguvu za nyuklia katika jeshi la
wanamaji la Marekani, pia nyambizi h7=iyo ina uwezo wa kubeba makombora ya 154
Tomahawk na meli nyambizi nyingine ndogo pamoja na wanajeshi 60,
Meli hiyo inayojulikana kwa jina USS Michigan, ambayo ina uwezo wa
kushambulia kwa makombora, inatarajiwa kujiunga na kundi jingine la meli za
kivita zinazoelekea eneo hilo, zikiongozwa na meli kubwa ya kubeba ndege ya
Carl Vinson.
0 comments:
Post a Comment