Kufuatia maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo kwa mwaka huu
kauli mbiu yake ni ‘tokomeza Malaria kabisa’ Waiziri wa Afya, maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amepiga marufuku vituo vyote vya afya vya
umma kuwalipishwa wananchi wanaokwenda kupima maambukizi ya ugonjwa wa Malaria
kwa kipimo cha MRDT. Pia ameongeza kuwa matibabu ya ugonjwa huo yatakuwa bure
vituo vya umma havitatakiwa kuwalipishwa wagonjwa wa Malaria kwa ajili ya dawa
za mseto (ALUU).
“Napenda kusisitiza vituo vya umma vinavyotumia vipimo vya MRDT kwa
wagonjwa wa Malaria, vipimo hivyo ni bure na pia mgonjwa asilipishwe fedha kwa
dawa za mseto ama Yule aliyelazwa kuchomwa sindano ya ugonjwa huo, Waganga
wakuu wa mikoa na wilaya hakikisheni kuanzia sasa manfuatilia wahudumu wote na
watakaokiuka agizo hili watachukuliwa hatua za kisheria” alisema Waziri Ummy
Pia waziri Ummy amewataka wananchi kutoa ushirikiano kuwafichua wahudumu
na vituo ambavyo vitakuwa vikitoza fedha kwa ajili ya vipimo na matbabu kwa
ajili ya ugonjwa wa Malaria kupitia kipimo cha MRDT, pia maabara binafsi ambazo
zipo kifedha zaidi zimetakiwa kutoa huduma hiyo kuacha tabia ya kuwaambia
wana maambukizi ya ugonjwa wa Malaria wakati hawana na badala yake kuanglia
zaidi maisha ya watu.
Waziri Ummy Mwalimu pia ametoa takwimu kutoka vituo vya afya
zinazoonesha kwamba takriban watu Milioni 12 kila mwaka wanaugua ugonjwa huo,
huku mkoa wa Kagera, Geit na Kigoma ikiongoza kwa maambukizi ya ugonjwa huo kwa
mwaka 2015 na 2016 ambapo watoto wenye umri chini ya miaka mitano na mama
wajawazito wakiathirika zaidi.
0 comments:
Post a Comment