Mamlaka ya mapato Tanzania (“TRA) imefanikiwa kukusanya Trilioni 10.87
hadi kufikia mwezi Machu mwaka huu wa fedha 2016/2017 ambapo pia malmaka hiyo
imesema kwa mwaka huu wa fedha 2016/2017 inatakiwa kukusanya Trilioni 15.105.
Maneno hayo yamesemwa na Kamishna Mkuuwa Mamlaka hiyo Chalres Edward Kichere
alipokuwa katika mahojiano na mtangazaji wa TBC1 Rashid Salum katika kipindi
cha Tunatekeleza.
Kichere aliongeza kwa kusema kuwa mpaka mwezi Juni mwaka 2017 TRA
itahakikisha inatimiza lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 15.105, alisema TRA
ina waajiriwa wapya ambao wamepata mafunzo kutoka chuo cha kodi juu ya
ukusanyaji kodi ambao wapo kwa ajili ya majukumu ya ukusanyaji wa kodi nchini
“Tunatumia mfumo wa TEHAMA kukusanya kodi na mifumo mwingine mbali mbali
kama vile Tigo Pesa, Airtel Money, na M-Pesa ili kurahisishia watu kulipa kodi
wakiwa majumbani na kuepuka usumbufu” alisema Kichere.
Kichere alisema mamlaka hiyo imeji[anga kuboresha mahusiano yake na
wafanyabiashara, kuhakikisha wanalipa kodi stahiki kwa mujibu wa sharia. Hata
hivyo Mamlaka hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa walipa kodi kupitia mitandao ya
kijamii na ziara mbali mbali.
0 comments:
Post a Comment