WANAMGAMBO WA ALSHABAB ZAIDI YA 50 WAUAWA NA JESHI LA KENYA


Wanamgambo zaidi ya 50 wa Al Shabab wauawa na jeshi la Kenya katika operesheni iliyofanywa kusini mwa Somalia. Jeshi la Kenya limesema lilinasa shehena ya silaha na risasi na kuharibu kabisa kambi ya wanamgambo hao katika Lower Juba,eneo la Badhaadhe.

Al Shabab wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Somalia, japo mpaka sasa kundi hilo halijazungumza lolote juu ya shambulio hilo.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment