Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira
Mhe. January Makamba, amesema kuwa changamoto za Muungano wa iliyokuwa
Tanganyika na Zanzibar zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka 15 mwaka 2006 hadi
kufikia changamoto 3 kwaka huu 2017, Muungano unaotimiza miaka 53 wiki ijayo.
Waziri
Makamba amezungumza hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa katika mkutano na waandishi
wa habari ulioandaliwa na waratibu wa sherehe za kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Walemavu na
kusimamiwa na Waziri Mwenye dhamana Mhe Jenista Mhagama.
Mhe. Makamba amezitaja changamoto zilizobakia kuwa ni pamoja na
usajili wa vyombo vya moto unaorahisisha kusafirisha magari kutoka Zanzibar
kwenda Bara na kutoka Bara kwenda Zanzibar na kusema kuwa swala hili linafanyiwa
kazi kwa kumalizwa kwa taratibu za kisheria.
Alisema kuwa changamoto nyingine inahusu Hisa za Zanzibar kwa
iliyokuwa bodi ya safari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Pamoja na Mapendekezo
ya tume ya Pamoja ya fedha.
Awali akizungumzia Muungano huo unaotimiza miaka 53, Waziri
Makamba Alisema kuwa umekuwepo kisheria na umerasimisha udugu na ushirikiano
uliyokuwepo kati ya Bara na Visiwani.
Mkutano huo wa waandishi wa habari uliandaliwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Walemavu umehudhuriwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Rugimbana, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wa Ofisi
hizo.
0 comments:
Post a Comment