TANGA YAENDELEZA VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Ndug Martin Shighela, amesema Vita ya madawa ya kulevya inaendelea hivyo kuviagiza vikosi vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha inawakamata vinara wa wasafirishaji na wauzaji.
Mkuu wa mkoa Martin Shighela akizungumza wakati wa hafla hiyo 
Akizungumza katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Comperence Centre (TICC), Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.
Alisema vijana wengi wamekuwa wakiathirika na matumizi ya madawa ya kulevya na Taifa kukosa nguvu kazi ya kuleta maendeleo na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha Tanga hakuna njia ya upitishaji.

“Kuna wagonjwa wa akili kutokana na maumbile yao lakini kuna wagonjwa wengine wa akili wa kujitakia ambao sababu zake ni matumizi ya madawa ya kulevya” alisema Shighela na kuongeza “Ili kuwaokoa vijana wetu na kupunguza nguvu kazi naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu ya mapambano ya madawa ya kulevya” alisema
Kwa upande wake Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Karstand, amewataka watumishi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo hilo kama ilivyo matumizi yake.
Alisema Serikali ya Norway itaisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kijamii ikiwemo Afya, elimu, Mazingira pamoja na wagonjwa wa Afya ya Akili.
Balozi wa Norway hapa nchini Hanne-Marie  akizungumza wakti wa hafla hiyo



Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment