Watu watatu wanaodaiwa kuwa
miongoni mwa waliohusika kuwaua viongozi wa vijiji na askari polisi nane katika
wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani wameuawa na jeshi la polisi
mkoani humo kwa kupigwa risasi.
Kamanda wa jeshi la polisi
mkoani Pwani Onesmo Lyanga amedai kuwa watu hao wamefariki dunia walipokuwa
wakipelekwa hospitali ya Mission ya Mchukwi kwa matibabu baada ya kujehiwa na
risasi miguuni na kiunoni.
Askari polisi waliamua kuchukua
uamuzi huo baada ya watu hao kukaidi amri halali ya polisi ya kuwataka wasimame
baada ya kuwatilia mashaka na kukimbilia porini wakiwa kwenye pikipiki, watu
hao walikuwa katika pikipiki tatu hukumbili kati ya hizo zilikuwa zimewabeba
watu waliovalia hijabu wakitokea Kibiti katika barabara kuu ya Dar-Lindi.
Kamanda Laynga ameeleza
kwamba askari wa kituo cha Mwembe Muhoro waliwasimamisha watu lakini walikaidi
amri hiyo, ndipo askari walipochukua hatua ya kuwafuatilia huku wakifyatua juu
risasi kuwaonya kabla ya watu hao kuruka kutoka kwenye pikipiki na kukimbilia
maporini, kitendo kilichowafanya askari kuwafyetulia risasi watu hao.
Kamanda pia ameongeza kuwa
watu hao waliokuwa wamevalia hijabu walitambulika kuwa walikuwa wanaume
waliotumia pikipiki aina ya Boxer yenye namba MC 272 BLW za usajili.
0 comments:
Post a Comment